Thursday, August 25, 2016

HIO NDOA WACHA IKAE

Mara nyingi utapata ndoa nyingi uwa zinashindwa kuendelea na mpaka maafa yanatokea pale wanandoa wameshindwa kukaa pamoja lakini unaona nikama wanalazimishwa kuishi ili kuziba aibu eti mwanangu ukirudi nyumbani watu watatucheka sisi wazazi wako.ukiweza kuskiza story za wanandoa na yale waschana wanayopitiwa kwenye ndoa zao uwezi kuamini kabisa.kuna mrembo moja ameniambia anapigwa sana na mume wake yani mume wake akija nyumbani jioni anaona kama ni jambazi na kumuambia rudi kwenu mie sikutaki.akirudi kwao ndugu zake wanamwambia rudi huko huko.sasa nauliza hadi mtakapo rudishiwa maiti nyumbani ndio mutajua kua alikua anapigwa.tumeona watu wakikatana sehemu za siri na mikono yani unarudi kwenu sehemu za mwili wako hamna je ni sawa kusubiria mpaka zifike hapo

No comments:

Post a Comment