Tuesday, April 29, 2014

MZIKI UNAITAJI KUPENDWA NAO UKUKUBALI.

For the last 14 years have been in the music industry i tell you its not easy as many  may think it is ,, safari hii inaitaji sana kujituma na unaposhikwa mkono mbele unaitaji kusema naweza kule mbele bila alienishika mkono ili kumpa nguvu alianza kukushika mkono.nyota ndogo ni madebe .madebe ni mtu amabae maishani mwangu siwezi kumsahau hata siku moja maana ndie alie nishika mkono na kunifanyia kila kitu yeye mwenyewe bila kusema kua nimetoa senti hata moja kwa kujenga jina hili..hata siku moja sikuwai kumkosea na iwapo niliwai basi nilikua mwepesi wakuomba msamaha ilifikia nimemkasirisha.madebe alipoondoka wengi walisema nyota ndogo kwisha hatutamsikia tena.nilika ndani ya moyo wangu nilijua kweli mimi kwisha.lakini maneno ya watu kuongea vibaya yalinijenga sana maana bila wao kujua yalinipa nguvu sana.nilitia bidii.shows nilizopiga baada ya madebe kuondoka zilikua kubwa mno na hapo nilianza kujua nguvu yangu kama nyota ndogo.nilijua kuitisha hela nazozitaka na nikapewa.mwanzoni nilikua sijui lakini badebe alikua akisema bei mimi nikuenda kupiga show.kwaivyo kuondoka kwake kulinitia uzuni sana upande mwengine ULINIPA NGUVU ZAIDI.nimejifunza heshima,ustarabu,uvumilivu,ubinafsi niliuweka kando,kunyenyekea hata palipo na madharau lakini yote najua lengo langu.nina watoto wawili na mimi ni single mum lakini sijawai kulia ngoa kuhusu maisha kwakua nakubali yalivyo bila kusema uongo eti mimi nina kile ama nina hiki na sina.wasani tukikubali kuishi maisha ya kawaida basi tutafika mbali sana..muimu ni nyimbo nzuri wenye ujumbe.tuapende mashabiki hata wanao tutukana tukiwa juu kwaani maana yule shabiki amekuja kukuona wewe na amelipa.usimrudishie matusi yale maana wengine wanatupima.mimi sio tajiri kama wengine wanavyodai.ila naishi maisha niyawezayo bila kuiga.yakawaida tu.siwezi kuishi nyali na siwezi kulipa nyali kisa mimi ni nyota ndogo watu watanicheka?watu gani?wanajua nakula nini ?hawajui kwaivyo binadamu wasikutie tumbo joto.kama uwezo wako wa elfu tano lipa hio hio.maana ukienda nyali alafu tukuone umerudi mtopanga tena watakucheka hao hao.HUSIA KWA WASANII WENZANGU.KULA TANO WEKA TANO .JUA NGUVU YAKO.ANAEKUSEMA KWA UBAYA NDIE ANAEKUPA NGUVU ZAIDI.HAKUNA KITU RAISI HAPA DUNIANI.KILA KITU NIKUJI KAKAMUA NA KWAUAKIKA UTAPATA UTAKACHO............... NARUDIA.MZIKI UNAITAJI  KUPENDWA NAO UKUKUBALI

No comments:

Post a Comment